MKURUGENZI MANISPAA YA KIGOMA UJIJI KUSHTAKIWA KUTOWALIPA WENYEVITI WA MITAA

Wenyeviti wa mitaa sitini na nane katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wameazimia kuishtaki halmashauri hiyo kwa kushindwa kualipa stahiki zao kwa zaidi ya miezi minane na wengine kudai madai ya zaidi ya miaka minne. Ucheleweshwaji wa malipo ya madai hayo umefanya wenyekiti hao kukutana kujadili mustakabali juu ya malipo hayo ikiwemo kwenda mahakamani